Aal-i-Imraan 3:179
آل عمرانمَّا كَانَ ٱللَّهُ لِيَذَرَ ٱلْمُؤْمِنِينَ عَلَىٰ مَآ أَنتُمْ عَلَيْهِ حَتَّىٰ يَمِيزَ ٱلْخَبِيثَ مِنَ ٱلطَّيِّبِ ۗ وَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيُطْلِعَكُمْ عَلَى ٱلْغَيْبِ وَلَـٰكِنَّ ٱللَّهَ يَجْتَبِى مِن رُّسُلِهِۦ مَن يَشَآءُ ۖ فَـَٔامِنُوا۟ بِٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦ ۚ وَإِن تُؤْمِنُوا۟ وَتَتَّقُوا۟ فَلَكُمْ أَجْرٌ عَظِيمٌ
Na hakuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwaacha Waumini katika hali mliyo nayo mpaka apambanue mbaya kutokana na mwema. Na wala hakuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwajulisha mambo ya ghaibu. Lakini Mwenyezi Mungu humteua katika Mitume wake amtakaye. Basi muaminini Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Na mkiamini, na mkamcha Mungu, basi mtakuwa na ujira mkubwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwaacha Waumini katika hali mliyo nayo mpaka apambanue wabaya na wema. Wala haiwi kwa Mwenyezi Mungu kukujuulisheni mambo ya ghaibu. Lakini Mwenyezi Mungu humteua katika Mitume wake amtakaye. Basi muaminini Mwenyezi Mungu na Mitume yake. Na mkiamini na mkamchamngu mtakuwa na ujira mkubwa. [179]
[179] Haiwi kuwa Mwenyezi Mungu akuacheni enyi jamaa Waumini katika hali mliyo nayo ya mchanganyiko wa Muumini na mnaafiki, mpaka awatenganishe baina yenu kwa misukosuko na taabu ili mumwone mnaafiki khabithi na Muumini mwema. Wala sio mwendo wa Mwenyezi Mungu kumjuulisha yeyote katika viumbe vyake khabari za ghaibu. Walakini Mwenyezi Mungu humteua katika Mitume yake ampendaye akamjuvya anacho kitaka katika mambo yake ya ghaibu. Na nyinyi mkiamini na mkamcha Mola wenu Mlezi kwa kujilazimisha kumt'ii atakutieni katika Pepo iwe ndio malipo. Na hayo ndio malipo yaliyo bora na makubwa kabisa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakuwa Allah Mtukufu ni Mwenye kuwaacha, enyi wenye kumuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na wenye kuzifuata Sheria Zake kivitendo, juu ya hivyo mlivyo ya kuchanganyikana mwenye Imani na mnafiki, mpaka Ampambanue muovu na mwema, ili ajulikane mnafiki na Muumini mkweli. Na haikuwa ni katika hekima ya Allah Mtukufu, enyi Waumini, kwamba Atawafunulia ghaibu Anayoijua kuhusu waja Wake, mkamjua Muumini kati yao na mnafiki. Lakini Yeye Anawapambanua kwa misukosuko na mitihani. Isipokuwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Anamteua Amtakaye katika wajumbe Wake ili kumuonesha ujuzi wa ghaibu kwa wahyi utokao Kwake. Basi muaminini Allah Mtukufu na Mtume Wake. Na iwapo mtaamini, imani ya kweli, na mkamuogopa Mola wenu kwa kumtii, mtapata malipo makubwa mbele ya Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net