Aal-i-Imraan 3:178
آل عمرانوَلَا يَحْسَبَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ أَنَّمَا نُمْلِى لَهُمْ خَيْرٌ لِّأَنفُسِهِمْ ۚ إِنَّمَا نُمْلِى لَهُمْ لِيَزْدَادُوٓا۟ إِثْمًا ۚ وَلَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ
Wala wasidhani kabisa wale wanaokufuru kwamba muhula huu tunaowapa ni heri kwao. Hakika, tunawapa muhula ili wazidishe dhambi. Na wana adhabu ya kudunisha.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala wasidhani wale wanao kufuru kwamba huu muhula tunao wapa ni kheri yao. Hakika tunawapa muhula wazidi madhambi. Na yao wao ni adhabu ya kuwadhalilisha. [178]
[178] Wasidhani hao makafiri kuwa vile kuwapururia tunapo wakunjulia umri wao, na tukawapa njia za starehe katika maisha yao ya duniani, kuwa ndio kheri yao. Kwani kuwaongezea umri na kuwakunjulia riziki huwapelekea kudumu na kuchuma madhambi na kuzidi kustahiki adhabu ya kuwafedhehesha aliyo waandalia Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wala wasidhani wakanushaji kwamba sisi tukiwarefushia umri wao, tukawastarehesha kwa starehe za duniani na tusiwaadhibu kwa ukafiri wao na madhambi yao kwamba watakuwa wamepata heri ya nafsi zao. Hakika tunawacheleweshea adhabu na ajali zao ili wazidishe dhuluma na ukiukaji mipaka. Na watapata adhabu yenye kuwadhalilisha.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net