Aal-i-Imraan 3:177
آل عمرانإِنَّ ٱلَّذِينَ ٱشْتَرَوُا۟ ٱلْكُفْرَ بِٱلْإِيمَـٰنِ لَن يَضُرُّوا۟ ٱللَّهَ شَيْـًٔا وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ
Hakika, wale walioununua ukafiri kwa Imani, hawatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu. Na wana adhabu chungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika wale walio nunua ukafiri kwa Imani hawatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu, na yao wao ni adhabu chungu. [177]
[177] Hakika watu hao walio khiari ukafiri badala ya Imani, wakatafuta ukafiri na wakaacha Imani, hawatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu, na watapata Akhera adhabu kali ya kutia uchungu mkubwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika wale walioibadili Imani kwa kufuata ukafiri, hawatamdhuru Allah Mtukufu chochote. Bali madhara ya kitendo chao yatawarudia wenyewe. Na huko Akhera watapata adhabu iumizayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net