Aal-i-Imraan 3:176
آل عمرانوَلَا يَحْزُنكَ ٱلَّذِينَ يُسَـٰرِعُونَ فِى ٱلْكُفْرِ ۚ إِنَّهُمْ لَن يَضُرُّوا۟ ٱللَّهَ شَيْـًٔا ۗ يُرِيدُ ٱللَّهُ أَلَّا يَجْعَلَ لَهُمْ حَظًّا فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ
Wala wasikuhuzunishe wale wanaoukimbilia ukafiri. Hakika, hao hawamdhuru kitu Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anataka asiwawekee fungu lolote katika Akhera. Na wana adhabu kubwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala wasikuhuzunishe wale wanao kimbilia ukafirini. Hakika hao hawamdhuru kitu Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anataka asiwawekee sehemu yoyote katika Akhera, na yao wao adhabu kubwa. [176]
[176] Ewe Nabii! Usihuzunike ukiwaona wale ambao wanazidi ukafiri, na wanawania kuzidisha maovu. Hao hawamletei Mwenyezi Mungu madhara yoyote, kwani Yeye ni Mwenye nguvu juu ya waja wake. Bali Mwenyezi Mungu anataka wasiwe na sehemu yoyote katika thawabu za Akhera, na juu ya kukosa kwao thawabu hizo njema watapata adhabu kubwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wasikutie huzuni moyoni mwako hawa makafiri, ewe Mtume, kwa kukimbilia kwao kukanusha na kuingia kwenye upotevu. Hakika wao, kwa hilo, hawatamdhuru Allah Mtukufu chochote. Hakika ni kwamba wao wazidhuru nafsi zao kwa kuzinyima utamu wa Imani na thawabu kubwa. Allah Mtukufu Anataka Asiwape malipo mema yoyote huko Akhera, kwa kuwa wao wamejiepusha na ulinganizi wa haki. Na wao watapata adhabu kali.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net