Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 175

Aal-i-Imraan 3:175

آل عمران

إِنَّمَا ذَٰلِكُمُ ٱلشَّيْطَـٰنُ يُخَوِّفُ أَوْلِيَآءَهُۥ فَلَا تَخَافُوهُمْ وَخَافُونِ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ

Maana

Hakika, huyo ni Shetani tu anawatia hofu marafiki zake. Basi msiwaogope. Bali niogopeni Mimi ikiwa nyinyi ni Waumini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika huyo ni Shet'ani anawatia khofu marafiki zake, basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi mkiwa nyinyi ni Waumini. [175]

[175] Mwenyezi Mungu Aliye takasika anawabainishia Waumini kwamba hao wanao kutieni khofu kuogopa kupambana na maadui zenu si lolote ila ni vibaraka wa Shetani anaye watia khofu wafwasi wake awafanye woga. Na nyinyi si katika hao. Basi msiridhie kutishwa, bali mkhofuni Mwenyezi Mungu peke yake kama nyinyi mna Imani ya kweli, na mnasimamia kutimiza yanayo lazimishwa na Imani hiyo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika anayewazorotesha nyinyi katika hilo ni Shetani. Amewajia kuwafanya nyinyi muwaogope wasaidizi wake. Basi msiwaogope washirikina, kwani wao ni wanyonge, hakuna mwenye kuwanusuru. Niogopeni mimi kwa kuelekea kwangu kwa utiifu, iwapo nyinyi kweli mnaniamini na mnamfuata Mtume wangu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net