Aal-i-Imraan 3:174
آل عمرانفَٱنقَلَبُوا۟ بِنِعْمَةٍ مِّنَ ٱللَّهِ وَفَضْلٍ لَّمْ يَمْسَسْهُمْ سُوٓءٌ وَٱتَّبَعُوا۟ رِضْوَٰنَ ٱللَّهِ ۗ وَٱللَّهُ ذُو فَضْلٍ عَظِيمٍ
Basi wakarudi na neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu na fadhila. Hakuna baya lililowagusa, na wakafuata yanayomridhisha Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kubwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi wakarudi na neema na fadhila za Mwenyezi Mungu. Hapana baya lilio wagusa, na wakafuata yanayo mridhi Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kuu. [174]
[174] Kisha wakatoka kwenda kwenye Jihadi na kupambana na hilo jeshi kubwa, lakini washirikina wakaingiwa na woga wakakimbia. Wakarejea Waumini kuwa wameshinda kwa neema ya salama ilhali wao wana hamu ya Jihadi, na wana malipo na thawabu na fadhila ya Mwenyezi Mungu kwao kwa vile kutia kitisho katika nyoyo za maadui zao, na wao wasipatikane na maudhi yoyote. Waliitafuta radhi ya Mwenyezi Mungu, na wao wakaistahiki fadhila yake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kubwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi wakarudi kutoka Ḥamrã’ al Asad kuja Madina wakiwa wana neema za Allah Mtukufu kwa kupata thawabu nyingi na nyongeza za daraja ya juu zitokazo Kwake, huku Imani na yakini zimeongezeka kwao, maadui wa Allah Mtukufu wamewadhalilisha, wamefaulu kwa kusalimika na kuuawa na kupigana, na wamefuata mambo ya kumridhisha Allah Mtukufu kwa kumtii Yeye na Mtume Wake. Na Allah Mtukufu ni Mwenye ihsani na vipawa vingi vyenye kuwaenea wao na wengineo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net