Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 173

Aal-i-Imraan 3:173

آل عمران

ٱلَّذِينَ قَالَ لَهُمُ ٱلنَّاسُ إِنَّ ٱلنَّاسَ قَدْ جَمَعُوا۟ لَكُمْ فَٱخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إِيمَـٰنًا وَقَالُوا۟ حَسْبُنَا ٱللَّهُ وَنِعْمَ ٱلْوَكِيلُ

Maana

Wale walioambiwa na watu: 'Hakika, kuna watu wamewakusanyikia, hivyo waogopeni!' Hayo yakawazidishia Imani, na wakasema: Mwenyezi Mungu anatutosha, naye ni mbora zaidi wa kutegemewa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Walio ambiwa na watu: Kuna watu wamekukusanyikieni, waogopeni! Hayo yakawazidishia Imani, wakasema: Mwenyezi Mungu anatutosha, naye ni mbora wa kutegemewa. [173]

[173] Hao ndio walio tiwa khofu na watu kwa kuwaambia: Maadui zenu wamekusanya jeshi kubwa kukupigeni, basi waogopeni. Na wao hawakudhoofika wala hawakulegea, bali walizidi Imani ya Mwenyezi Mungu na wakawa na moyo kuwa atawanusuru. Jawabu yao ikawa: Mwenyezi Mungu anatutosheleza. Yeye ndiye aliye tawala mambo yetu. Na Yeye ndiye anaye tegemezwa mambo yote.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wao ni wale walioambiwa na baadhi ya washirikina, «Abu Sufyani na wenzake wameamua kuwarudia nyinyi ili kuwamaliza, basi jihadharini nao na mjikinge na kukutana nao, kwani hamna nguvu za kupambana nao.» Tahadhari hiyo iliwazidishia yakini na kuikubali kikweli ahadi ya Allah Mtukufu kwao na haikuwazuia na uamuzi wao. Hapo walikwenda wakielekea pale Allah Mtukufu Alipotaka na wakasema, «Ḥasbunã Allãh wa Ni’ma al Wakîl» Yaani, Mtosheleza wetu ni Allah Mtukufu na Yeye Ndiye Wakili mwema Mwenye kutegemezewa mipango ya waja Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net