Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 172

Aal-i-Imraan 3:172

آل عمران

ٱلَّذِينَ ٱسْتَجَابُوا۟ لِلَّهِ وَٱلرَّسُولِ مِنۢ بَعْدِ مَآ أَصَابَهُمُ ٱلْقَرْحُ ۚ لِلَّذِينَ أَحْسَنُوا۟ مِنْهُمْ وَٱتَّقَوْا۟ أَجْرٌ عَظِيمٌ

Maana

Wale waliomwitikia Mwenyezi Mungu na Mtume baada ya kwishapatwa na majeraha. Kwa waliofanya wema miongoni mwao na wakamcha Mungu, utakuwa ujira mkubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Walio mwitikia Mwenyezi Mungu na Mtume baada ya kwisha patwa na majaraha - kwa walio fanya wema miongoni mwao na wakamchamungu utakuwa ujira mkubwa. [172]

[172] Waumini hao ni wale ambao wameitikia wito wa Mtume wa kuanza upya Jihadi baada ya pigo kubwa walilo lipata katika vita vya Uhud. Kwa hivyo basi wakawa ni wenye kutenda wema, na wakajilinda na kuasi amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Basi wakastahiki ujira mkubwa katika Nyumba ya Malipo na Neema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wale waliouitikia mwito wa Allah Mtukufu na Mtume wake na wakatoka kuwafuata washirikina mpaka kijiji cha Ḥamrã’ al-Asad baada ya kushindwa katika vita vya Uḥud, pamoja na maumivu na majaraha waliyokuwa nayo, wakafanya upeo wa juhudi zao na wakashikamana na mwongozo wa Mtume wao, basi watenda wema hao na wacha Mungu hao watapata thawabu kubwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net