Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 171

Aal-i-Imraan 3:171

آل عمران

يَسْتَبْشِرُونَ بِنِعْمَةٍ مِّنَ ٱللَّهِ وَفَضْلٍ وَأَنَّ ٱللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ ٱلْمُؤْمِنِينَ

Maana

Wanapata bishara ya neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu na fadhila, na ya kwamba Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa Waumini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wanashangilia neema na fadhila za Mwenyezi Mungu, na ya kwamba Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa Waumini. [171]

[171] Nyuso za Mashahidi zinameremeta kwa neema ya kufa shahidi na neema ya Pepo, na ubora wa karama, na ya kwamba haupotei ujira wa Waumini.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika wao watakuwa wamejawa na furaha kwa neema za Allah Mtukufu na vipawa Vyake vingi na hakika Allah Mtukufu Hayapotezi malipo ya wenye kumuamini, bali Anayakuza na kuyaongeza kwa fadhila Zake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net