Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 170

Aal-i-Imraan 3:170

آل عمران

فَرِحِينَ بِمَآ ءَاتَىٰهُمُ ٱللَّهُ مِن فَضْلِهِۦ وَيَسْتَبْشِرُونَ بِٱلَّذِينَ لَمْ يَلْحَقُوا۟ بِهِم مِّنْ خَلْفِهِمْ أَلَّا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ

Maana

Wanafurahia yale aliyowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila zake, na wanawapa bishara wale ambao bado hawajajiunga nao, walio nyuma yao, ya kwamba haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wanafurahia aliyo wapa Mwenyezi Mungu kwa fadhila yake, na wanawashangilia wale ambao bado hawajajiunga nao, walio nyuma yao, ya kwamba haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika. [170]

[170] Nyuso zao zinameremeta kwa furaha na bishara kwa fadhila ya pekee aliyo wapa Mwenyezi Mungu, na wanawafurahia ndugu zao ambao walio waacha duniani wangali wahai, wanashika mwendo wa Imani na Jihadi, na ya kwamba hapana khofu juu yao kupata lolote la karaha wala si wenye kuhuzunika kwa kumkosa mpendwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Furaha iliwaenea, wakati Mola wao Alipowaneemesha na kuwapa neema na radhi zenye kuwaliwaza macho yao, zikiwa ni miongoni mwa ukarimu Wake na takrima Yake. Watakuwa wakiwafurahia ndugu zao wenye kupigana jihadi waliowaacha duniani wakiwa hai, wakiwatarajia wafaulu kama walivyofaulu wao. Kwa kuwa wao waelewa kwamba hao ndugu zao, waliowaacha duniani wakiwa hai, watapata heri waliyoipata wao, iwapo watakufa mashahidi katika njia ya Allah Mtukufu hali ya kumtakasia Yeye, na kwamba hawatakuwa na chochote cha kuogopa kuhusu mambo ya mustakbali wao huko Akhera wanayoyakabili wala hawatakuwa na huzuni juu ya yale yaliyowapita wakayakosa ya hadhi za kilimwengu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net