Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 169

Aal-i-Imraan 3:169

آل عمران

وَلَا تَحْسَبَنَّ ٱلَّذِينَ قُتِلُوا۟ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ أَمْوَٰتًۢا ۚ بَلْ أَحْيَآءٌ عِندَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ

Maana

Wala kabisa usiwadhanie wale waliouliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni wafu. Bali hao wa hai kwa Mola wao Mlezi wanaruzukiwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala kabisa usiwadhanie walio uliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni maiti. Bali hao ni wahai, wanaruzukiwa kwa Mola wao Mlezi. [169]

[169] Wala usidhani kabisa kuwa walio uliwa katika Njia ya Mwenyezi Mungu ni maiti, bali hao wahai kwa uhai anao ujua Mwenyewe Mwenyezi Mungu, wanaruzukiwa kwa Mola wao Mlezi, riziki njema anayo ijua Yeye.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wala usidhani, ewe Mtume, kwamba wale waliouawa katika njia ya Allah Mtukufu ni wafu hawahisi chochote. Bali wao wako hai uhai wa barzakh kwenye ujirani wa Mola wao Ambaye walipigana jihadi kwa ajili Yake na wakafa katika njia Yake, inawapitia riziki yao huko Peponi na wananeemeshwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net