Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 168

Aal-i-Imraan 3:168

آل عمران

ٱلَّذِينَ قَالُوا۟ لِإِخْوَٰنِهِمْ وَقَعَدُوا۟ لَوْ أَطَاعُونَا مَا قُتِلُوا۟ ۗ قُلْ فَٱدْرَءُوا۟ عَنْ أَنفُسِكُمُ ٱلْمَوْتَ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ

Maana

Wale waliowaambia ndugu zao, na wao wenyewe walikuwa wamekaa: Lau wangelitutii, wasingeliuliwa. Sema: Ziondoleeni nafsi zenu mauti kama nyinyi ni wakweli.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hao ndio walio waambia ndugu zao na wao wenyewe wakakaa kitako: Lau wengeli tut'ii wasingeli uliwa. Sema: Ziondoleeni nafsi zenu mauti kama mnasema kweli. [168]

[168] Na hao ndio walio baki nyuma wesende vitani wakakwepa, na wakasema kwa mintarafu ya ndugu zao walio toka wakauliwa: Lau wangeli tufuata sisi wakakaa nyuma kama tulivyo kaa sisi wangeli okoka kama tulivyo okoka. Waambie: Zizuieni nafsi zenu basi zisife, kama mnasema kweli kuwa hadhari inazuia kadari.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wanafiki hawa ndio wale waliokaa wakawaambia ndugu zao waliopata msiba pamoja na Waislamu kwenye vita vyao na washirikina siku ya Uḥud, «Lau kama watu hawa wangalitutii hawangaliuawa.» Sema, ewe Mtume, uwaambie «Zizuieni nafsi zenu na kifo, ikiwa nyinyi ni wa kweli katika madai yenu kwamba wao kama wangaliwatii hawangaliuawa na kwamba mumeokoka na mauti kwa kukaa kwenu kutokwenda vitani».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net