Aal-i-Imraan 3:167
آل عمرانوَلِيَعْلَمَ ٱلَّذِينَ نَافَقُوا۟ ۚ وَقِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا۟ قَـٰتِلُوا۟ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ أَوِ ٱدْفَعُوا۟ ۖ قَالُوا۟ لَوْ نَعْلَمُ قِتَالًا لَّٱتَّبَعْنَـٰكُمْ ۗ هُمْ لِلْكُفْرِ يَوْمَئِذٍ أَقْرَبُ مِنْهُمْ لِلْإِيمَـٰنِ ۚ يَقُولُونَ بِأَفْوَٰهِهِم مَّا لَيْسَ فِى قُلُوبِهِمْ ۗ وَٱللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا يَكْتُمُونَ
Na ili awajue wale waliofanya unafiki, walipoambiwa: Njooni mpigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu au lindeni. Wakasema: 'Tungelijua kuna kupigana vita, bila ya shaka tungeliwafuata.' Wao siku ile walikuwa karibu zaidi na ukafiri kuliko Imani. Wanasema kwa midomo yao yasiyokuwa katika nyoyo zao. Na Mwenyezi Mungu anajua vyema wanayoyaficha.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ili awapambanue walio kuwa wanaafiki, wakaambiwa: Njooni mpigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu au lindeni. Wakasema: Tungeli jua kuna kupigana bila ya shaka tungeli kufuateni. Wao siku ile walikuwa karibu na ukafiri kuliko Imani. Wanasema kwa midomo yao yasiyo kuwamo nyoyoni mwao. Na Mwenyezi Mungu anajua kabisa wanayo yaficha. [167]
[167] Na hayo ili pia udhihiri unaafiki wa wanaafiki. Nao hawa ni wale walipo kuwa wanaondoka wanaacha vita wakaambiwa: Njooni mpigane kwa kumt'ii Mwenyezi Mungu, au kwa ajili ya kujilinda nafsi zenu. Wakasema: Lau kuwa tunajua kuwa mtakutana na vita, tungeli kwenda nanyi. Na wao walipo sema kauli hiyo walikuwa karibu zaidi na ukafiri kuliko Imani. Wanasema kwa midomo yao: Huko hakuna vita. Na hali wanaitakidi ndani ya nyoyo zao kuwa vita kweli vitakuwepo. Na Mwenyezi Mungu anajua vyema unaafiki wanao uficha, kwani Yeye anajua matokeo ya siri zao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na ili Awapambanue wanafiki ambao Allah Mtukufu Ameyafungua wazi yaliyomo ndani ya nyoyo zao, walipokuwa Waumini wawaambia, «Njooni mpigane pamoja na sisi katika njia ya Allah Mtukufu au kuweni ni msaada kwetu kwa kutufanya tuwe wengi.» Wakasema, «Lau kama tunajua kuwa nyinyi mtapigana na yoyote tungalikuwa na nyinyi dhidi yao.» Wao katika ukafiri, siku hii ya leo, wako karibu zaidi kuliko kuwa wao wako karibu na Imani.Kwani wao wanayasema kwa midomo yao yasiokuwa kwenye nyoyo zao. Na Allah Mtukufu Anayajua zaidi wanayoyaficha vifuani mwao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net