Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 166

Aal-i-Imraan 3:166

آل عمران

وَمَآ أَصَـٰبَكُمْ يَوْمَ ٱلْتَقَى ٱلْجَمْعَانِ فَبِإِذْنِ ٱللَّهِ وَلِيَعْلَمَ ٱلْمُؤْمِنِينَ

Maana

Na yale yaliyowapata siku yalipokutana makundi mawili, yalikuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na ili awajue Waumini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na yaliyo kusibuni siku yalipo pambana majeshi mawili yalikuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na ili awajue Waumini. [166]

[166] Enyi Waumini! Yaliyo kusibuni lilipo pambana jeshi lenu na jeshi la Washirikina katika Uhud yametokana kwa hukumu ya Mwenyezi Mungu, na ili awadhihirishie watu Imani ya Waumini ya kweli aliyo ifunza.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na yale yaliyotokea kwenu ya majaraha au ya mauaji katika vita vya Uḥud, siku ulipokutana mkusanyiko wa Waumini na mkusanyiko wa washirikina, na ukawa ushindi, mwanzo wa vita, ni wa Waumini kisha, mara ya pili, ukawa ni wa washirikina, yote hayo yalikuwa kwa uamuzi wa Allah Mtukufu na mpango Wake, ili yajitokeze yale Aliyoyajua Allah Mtukufu tangu kale, ili Awapambanue Waumini wa kweli miongoni mwenu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net