Aal-i-Imraan 3:165
آل عمرانأَوَلَمَّآ أَصَـٰبَتْكُم مُّصِيبَةٌ قَدْ أَصَبْتُم مِّثْلَيْهَا قُلْتُمْ أَنَّىٰ هَـٰذَا ۖ قُلْ هُوَ مِنْ عِندِ أَنفُسِكُمْ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ
Nyinyi mlipopatwa na msiba ambao nyinyi mmekwishawatia mara mbili mfano wake, mkasema: Umetoka wapi huu? Sema: Huo umetoka kwenu wenyewe. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Nyinyi - ulipo kusibuni msiba ambao nyinyi mmekwisha watia mara mbili mfano wa huo - mnasema: Umetoka wapi huu? Sema: Huo umetoka kwenu wenyewe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu. [165]
[165] Hivyo mnapigwa na mshangao na kuemewa pale yalipo kupateni siku ya Uhud masaibu ambayo nyinyi mlikwisha wapa maadui mara mbili mfano wa hayo katika siku ya Badri, hata mnasema kwa mastaajabu: Yamekuwaje mauwaji haya na kushindwa huku, na sisi ni Waislamu na Mtume wa Mwenyezi Mungu yuko nasi? Sema: Yaliyo kupateni yametokana na nafsi zenu kwa vile mlivyo mkhalifu Mtume. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu, naye amekulipeni kwa mujibu wa mlivyo tenda.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwa nini mlipopatwa na msiba uliowakumba siku ya Uḥud, ingawa mumewapata washirikina mara mbili yake siku ya Badr, mlisema kwa kustaajabu, «Mambo haya yatakuwa vipi, na sisi ni Waislamu, Mtume wa Allah Mtukufu yuko na sisi, na hawa ni washirikina?» Sema uwaambie, ewe Nabii, «Haya yaliyowapata yamesababishwa na nyinyi wenyewe kwa kuenda kinyume kwenu na amri ya Mtume wenu na kuelekea kwenu kukusanya ngawira.» Kwa hakika, Allah Mtukufu Anafanya Atakalo na Anahukumu Atakavyo. Hakuna mwenye kuitengua hukumu Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net