Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 184

Aal-i-Imraan 3:184

آل عمران

فَإِن كَذَّبُوكَ فَقَدْ كُذِّبَ رُسُلٌ مِّن قَبْلِكَ جَآءُو بِٱلْبَيِّنَـٰتِ وَٱلزُّبُرِ وَٱلْكِتَـٰبِ ٱلْمُنِيرِ

Maana

Na wakikukadhibisha, basi walikadhibishwa Mitume wengine kabla yako, waliokuja na hoja zilizo wazi, na Vitabu vyenye hekima, na Kitabu chenye nuru.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wakikukanusha basi walikanushwa Mitume wengine kabla yako walio kuja na hoja waziwazi na Vitabu vyenye hikima, na Kitabu chenye Nuru. [184]

[184] Ikiwa watakukadhibisha, Ewe Nabii, wewe usisikitike. Kabla yako wamekutangulia wengi walio kadhibishwa na watu wao kwa chuki na inda, juu ya kuwa walikuja na dalili zilizo nyooka, na Vitabu vya mbinguni vyenye kuthibitisha ukweli wa Ujumbe wao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi ikiwa Mayahudi hawa na makafiri wengineo watakukanusha, ewe Mtume, hakika wabatilifu wamewakanusha Mitume wengi kabla yako waliowajia kaumu zao kwa miujiza mingi yenye kushinda, hoja zilizo wazi, vitabu vya mbinguni ambavyo ni nuru inayoondosha giza na Kitabu chenye ufafanuzi, kilicho wazi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net