Aal-i-Imraan 3:145
آل عمرانوَمَا كَانَ لِنَفْسٍ أَن تَمُوتَ إِلَّا بِإِذْنِ ٱللَّهِ كِتَـٰبًا مُّؤَجَّلًا ۗ وَمَن يُرِدْ ثَوَابَ ٱلدُّنْيَا نُؤْتِهِۦ مِنْهَا وَمَن يُرِدْ ثَوَابَ ٱلْـَٔاخِرَةِ نُؤْتِهِۦ مِنْهَا ۚ وَسَنَجْزِى ٱلشَّـٰكِرِينَ
Na haikuwa kwa nafsi kufa isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu kama ilivyoandikiwa muda wake. Na mwenye kutaka malipo ya duniani, tutampa kwayo. Na mwenye kutaka malipo ya Akhera, tutampa kwayo. Na tutawalipa wenye kushukuru.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na haiwezi nafsi kuwa ife ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu kama ilivyo andikwa ajali yake. Na mwenye kutaka malipo ya duniani tutampa; na mwenye kutaka malipo ya Akhera tutampa. Na tutawalipa wenye kushukuru. [145]
[145] Hayumkini mtu kufa ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Naye amekwisha viandikia viumbe ajali yao. Na atakaye starehe ya dunia Mwenyezi Mungu atampa, na atakaye malipo ya Akhera atayapata. Na Mwenyezi Mungu atawalipa wanao shukuru neema yake wakamt'ii kwa aliyo waamrisha ikiwa ni kupigana Jihadi au mengineyo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakuna yoyote atakayekufa isipokuwa kwa idhini ya Allah Mtukufu na makadirio Yake na mpaka aufikishe muda ambao Allah Mtukufu Amempangia. Hayo ni maandishi yaliyopangiwa wakati. Na yoyote ambaye kwa vitendo vyake anataka manufaa ya duniani, tutampa tulichomgawia cha riziki, na hatakuwa na fungu lolote kesho Akhera. Na yoyote ambaye anataka kwa vitendo vyake malipo ya Allah Mtukufu huko Akhera, tutampa kile alichokitaka na tutampa malipo yake kamili pamoja na fungu lake duniani la riziki alilogawiwa. Kwani huyu kwa utiifu wake na jihadi yake ametushukuru; na wenye kushukuru tutawalipa mema.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net