Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 146

Aal-i-Imraan 3:146

آل عمران

وَكَأَيِّن مِّن نَّبِىٍّ قَـٰتَلَ مَعَهُۥ رِبِّيُّونَ كَثِيرٌ فَمَا وَهَنُوا۟ لِمَآ أَصَابَهُمْ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ وَمَا ضَعُفُوا۟ وَمَا ٱسْتَكَانُوا۟ ۗ وَٱللَّهُ يُحِبُّ ٱلصَّـٰبِرِينَ

Maana

Na ni Manabii wangapi ambao Waumini wengi wenye ikhlasi walipigana vita pamoja nao! Na hawakulegea kwa yaliyowapata katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawakudhoofika wala hawakusalimu amri. Na Mwenyezi Mungu huwapenda wanaosubiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Manabii wangapi walipigana na pamoja nao Waumini wengi wenye ikhlasi! Hawakufanya woga kwa yaliyo wasibu katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawakudhoofika wala hawakuwa wanyonge. Na Mwenyezi Mungu huwapenda wanao subiri. [146]

[146] Na Manabii wangapi wamepigana vita na pamoja nao Waumini wengi wenye ikhlasi kwa Mola wao Mlezi! Nyoyo zao hazikuingia woga, wala azma zao hazikudahadari, wala hawakuwanyenyekea maadui zao kwa sababu ya masaibu yaliyo wapata katika Sabili Llahi, Njia ya Mwenyezi Mungu. Haya ni kwa sababu wamo katika ut'iifu wake, na Mwenyezi Mungu huwalipa wanao vumilia ikiwafika balaa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wengi kati ya Mitume waliotangulia, walipigana pamoja nao makundi mengi ya watu waliowafuata. Hawakudhoofika kwa yale yaliyowapata ya majaraha au mauaji, kwani hayo yalikuwa katika njia ya Mola wao. Wala hawakulemewa wala hawakumnyenyekea adui yao, bali walisubiri kwa yaliyowapata. Na Allah Mtukufu Anawapenda wenye kusubiri.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net