Aal-i-Imraan 3:147
آل عمرانوَمَا كَانَ قَوْلَهُمْ إِلَّآ أَن قَالُوا۟ رَبَّنَا ٱغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَإِسْرَافَنَا فِىٓ أَمْرِنَا وَثَبِّتْ أَقْدَامَنَا وَٱنصُرْنَا عَلَى ٱلْقَوْمِ ٱلْكَـٰفِرِينَ
Na haikuwa kauli yao isipokuwa walisema: Mola wetu Mlezi! Tufutie dhambi zetu na kupita kwetu kiasi katika mambo yetu, na isimamishe imara miguu yetu na utunusuru dhidi ya kaumu ya makafiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala kauli yao haikuwa ila ni kusema: Mola wetu Mlezi! Tughufirie madhambi yetu na kupita kwetu kiasi katika mambo yetu, na isimamishe imara miguu yetu na utunusuru tuwashinde kaumu ya makafiri. [147]
[147] Na kauli yao vilipo kuwa vita vikali haikuwa ila kusema: Mola wetu Mlezi! Tusamehe dhambi zetu kubwa na ndogo. Na tusimamishe imara katika midani za vita, na utunusuru na hawa maadui wa Dini yako, wenye kukukanya Wewe na ujumbe wa Mtume wako.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na halikuwa neno la hawa wenye kusubiri isipokuwa ni kusema, «Ewe Mola wetu! Tusamehe madhambi yetu na yaliyotokea kwetu ya kuruka mipaka katika mambo ya dini yetu na uzithibitishe nyayo zetu, tusipate kukimbia tunapopigana na adui yetu na utunusuru na yule anayepinga umoja wako na unabii wa Manabii wako».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net