Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 148

Aal-i-Imraan 3:148

آل عمران

فَـَٔاتَىٰهُمُ ٱللَّهُ ثَوَابَ ٱلدُّنْيَا وَحُسْنَ ثَوَابِ ٱلْـَٔاخِرَةِ ۗ وَٱللَّهُ يُحِبُّ ٱلْمُحْسِنِينَ

Maana

Basi Mwenyezi Mungu akawapa malipo ya duniani na malipo bora ya Akhera. Na Mwenyezi Mungu anawapenda wafanyao mema.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi Mwenyezi Mungu akawapa malipo ya duniani na bora ya malipo ya Akhera. Na Mwenyezi Mungu anawapenda wafanyao mema. [148]

[148] Mwenyezi Mungu akawapa ushindi na tawfiqi katika dunia, na akawadhaminia malipo mema kwa Akhera. Na Mwenyezi Mungu huwalipa wale wafanyao vitendo vyema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi Aliwapa Allah Mtukufu, wale wenye kusubiri, malipo yao duniani kwa kuwanusuru na maadui zao, kwa kuwafanya wakae kwa utulivu katika ardhi na kwa malipo mema yaliyo makubwa Akhera, nayo ni mabustani ya Peponi yaliyojaa neema. Na Allah Mtukufu Anampenda kila mtenda wema katika kumuabudu Mola wake na kuamiliana kwake na viumbe Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net