Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 149

Aal-i-Imraan 3:149

آل عمران

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِن تُطِيعُوا۟ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ يَرُدُّوكُمْ عَلَىٰٓ أَعْقَـٰبِكُمْ فَتَنقَلِبُوا۟ خَـٰسِرِينَ

Maana

Enyi mlioamini! Ikiwa mtawatii wale waliokufuru, watawarudisha kwa visigino vyenu, na hapo mtageuka huku mmehasirika.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio amini! Ikiwa mtawat'ii walio kufuru watakurudisheni nyuma, na hapo mtageuka kuwa wenye kukhasiri. [149]

[149] Enyi mlio amini! Mkiwat'ii maadui zenu makafiri, walio tangaza ukafiri wao au wakauficha, kwa hayo wanayo kuitieni kwa maneno au vitendo, watakuja kugeuzeni muingie ukafirini. Na hapo tena itakuwa mmekhasiri dunia na Akhera.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkazifuata sheria Zake kivitendo! Iwapo mtawatii walioukanusha uungu wangu na wasiwaamini Mitume wangu, miongoni mwa Mayahudi, Wanaswara, wanafiki na washirikina, katika yale wanayowaamrisha nyinyi nayo na wanayowakataza nyinyi nayo, watawapoteza njia ya haki na mtaritadi muache dini yenu na mrudi na hasara iliyo wazi na maangamivu ya kikweli.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net