Aal-i-Imraan 3:150
آل عمرانبَلِ ٱللَّهُ مَوْلَىٰكُمْ ۖ وَهُوَ خَيْرُ ٱلنَّـٰصِرِينَ
Bali Mwenyezi Mungu ndiye Kipenzi Mlinzi wenu. Naye ndiye mbora wa wanaonusuru.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Bali Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wenu, naye ndiye bora wa wasaidizi. [150]
[150] Mwenyezi Mungu ndiye wa kukunusuruni, basi msiwaogope hao binaadamu wenzenu, kwani Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa kunusuru.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika wao hawatawanusuru nyinyi; bali Allah Mtukufu Ndiye Mwenye kuwanusuru na Ndiye Mnusuru bora Asiyehitajia nusura ya mtu Mwengine.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net