Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 151

Aal-i-Imraan 3:151

آل عمران

سَنُلْقِى فِى قُلُوبِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ ٱلرُّعْبَ بِمَآ أَشْرَكُوا۟ بِٱللَّهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِۦ سُلْطَـٰنًا ۖ وَمَأْوَىٰهُمُ ٱلنَّارُ ۚ وَبِئْسَ مَثْوَى ٱلظَّـٰلِمِينَ

Maana

Tutatia hofu katika nyoyo za wale waliokufuru kwa vile walivyomshirikisha Mwenyezi Mungu na yale ambayo hakuyateremshia hoja yoyote. Na makazi yao ni Motoni. Na maovu mno ni maskani ya madhalimu!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Tutazitia khofu nyoyo za walio kufuru kwa vile walivyo mshirikisha Mwenyezi Mungu na washirika ambao hakuwateremshia hoja yoyote. Na makaazi yao ni Motoni; na maovu yaliyoje maskani ya wenye kudhulumu! [151]

[151] Yasikutieni unyonge yaliyo kupateni siku ya Uhud. Sisi tutaingiza khofu na vitisho katika nyoyo za maadui zenu kwa kuwa wao wamemshirikisha Mwenyezi Mungu na miungu mengine ambayo Mwenyezi Mungu hakuwateremshia hoja yoyote. Kwani Miungu hiyo hainufaishi wala haidhurishi kitu. Na makao yao yatakuwa Motoni Akhera, na maovu mno hayo makao ya madhaalimu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Tutatia fazaa na hofu kubwa katika nyoyo za waliokufuru, kwa sababu ya kumshirikisha kwao Allah Mtukufu na wale wanaodaiwa kuwa ni waungu. Wao hawana dalili au hoja kuwa waungu hao wana haki ya kuabudiwa pamoja na Allah Mtukufu. Basi hali yao hapa duniani ni papatiko na babaiko kwa kuwaogopa Waumini. Ama mahali pao watakaposhukia Akhera ni Moto. Na hili ni kwa sababu ya udhalimu wao na uadui wao. Na makao maovu kwao ni makao haya.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net