Aal-i-Imraan 3:144
آل عمرانوَمَا مُحَمَّدٌ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ ٱلرُّسُلُ ۚ أَفَإِي۟ن مَّاتَ أَوْ قُتِلَ ٱنقَلَبْتُمْ عَلَىٰٓ أَعْقَـٰبِكُمْ ۚ وَمَن يَنقَلِبْ عَلَىٰ عَقِبَيْهِ فَلَن يَضُرَّ ٱللَّهَ شَيْـًٔا ۗ وَسَيَجْزِى ٱللَّهُ ٱلشَّـٰكِرِينَ
Na Muhammad si isipokuwa Mtume tu. Wamekwishapita kabla yake Mitume. Je, akifa au akiuawa, mtageuka mrudi kwa visigino vyenu? Na atakayegeuka akarudi kwa visigino vyake, basi huyo hatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu atawalipa wanaoshukuru.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Muhammad hakuwa ila ni Mtume tu. Wamekwisha pita kabla yake Mitume. Je, akifa au akauwawa ndiyo mtageuka mrudi nyuma? Na atakaye geuka akarudi nyuma huyo hatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu atawalipa wanao mshukuru. [144]
[144] Katika vita vya Uhud ulitoka uvumi kuwa ati Mtume Muhammad s.a.w. kauwawa. Baadhi ya Waislamu walidahadari wakaingiwa kiwewe wakataka kurtadi, kuuacha Uislamu. Mwenyezi Mungu aliwakaripia kwa kuwaambia: Muhammad si chochote ila ni Mtume tu, na kabla yake wamekufa Mitume mfano wake yeye. Naye atakufa kama walivyo kufa wao, na atapita kama wao walivyo pita. Je, akifa au akauliwa ndio mtarejea nyuma kwenye ukafiri wenu? Na mwenye kurejea kwenye ukafiri baada ya kwisha amini, basi hatomdhuru kitu Mwenyezi Mungu, ila atakuwa anajidhuru nafsi yake kwa kujipeleka kwenye mateso. Na Mwenyezi Mungu atawalipa malipo mema wale wenye kusimama imara juu ya Uislamu, wenye kuishukuru neema yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakuwa Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, ni kiumbe aina nyingine, isipokuwa yeye ni Mtume wa jinsi ya Mitume wengine waliokuweko kabla yake, afikisha ujumbe wa Mola wake. Basi iwapo atakufa, kwa kumalizika muda wake, au atauawa, kama walivyoeneza uvumi maadui, kwani mtarudi nyuma na kuacha dini yenu na kuyaacha aliyowaletea Mtume wenu? Basi yoyote miongoni mwenu atakayerudi nyuma akaiacha dini yake, yeye hatamdhuru Allah Mtukufu chochote, bali ataidhuru nafsi yake madhara makubwa. Ama atakayekuwa na msimamo imara juu ya Imani yake na akamshukuru Mola wake juu ya neema ya Uislamu, hakika Allah Mtukufu Atamlipa malipo mazuri kabisa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net