Aal-i-Imraan 3:143
آل عمرانوَلَقَدْ كُنتُمْ تَمَنَّوْنَ ٱلْمَوْتَ مِن قَبْلِ أَن تَلْقَوْهُ فَقَدْ رَأَيْتُمُوهُ وَأَنتُمْ تَنظُرُونَ
Na nyinyi mlikuwa mkiyatamani mauti kabla hamjakutana nayo. Basi sasa mmekwishayaona na huku mnayatazama.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na nyinyi mlikuwa mkitamani mauti kabla hamjakutana nayo. Basi sasa mmekwisha yaona na huku mnayatazama. [143]
[143] Nyinyi mlikuwa mkitaka kufa katika Njia ya Mwenyezi Mungu kabla hamjayaona mauti na mkajua kitisho chake. Sasa basi nyinyi mmekwisha yaona mauti walipo uliwa ndugu zenu mbele yenu nanyi mnaangalia.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kwa hakika mlikuwa, enyi Waumini, kabla ya vita vya Uḥud mnatamani kukutana na maadui zenu, ili mpate utukufu wa jihadi na kufa mashahidi katika njia ya Allah Mtukufu ambao walibahatika nao ndugu zenu kwenye vita vya Badr. Basi hilo ndilo, limeshapatikana kwenu, mlilolitamani na mkaliomba. Basi jitokezeni mpigane na msubirishane.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net