Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 142

Aal-i-Imraan 3:142

آل عمران

أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تَدْخُلُوا۟ ٱلْجَنَّةَ وَلَمَّا يَعْلَمِ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ جَـٰهَدُوا۟ مِنكُمْ وَيَعْلَمَ ٱلصَّـٰبِرِينَ

Maana

Je, mnadhani kwamba mtaingia Bustanini ilhali Mwenyezi Mungu hajawajua wale miongoni mwenu waliopigana Jihadi, na akawajua waliosubiri?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Mnadhani mtaingia Peponi na hali Mwenyezi Mungu hajawapambanua wale miongoni mwenu walio pigana Jihadi, na hajawapambanua walio subiri? [142]

[142] Enyi Waumini! Msidhani kuwa mtaingia Peponi bila ya kubainika kati yenu wepi Mujahidiina, Wapigania Haki, wenye kusubiri na kuvumilia ambao wanat'ahirishwa na misukusuko na shida.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi Maswahaba wa Mtume Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie! Kwani mnadhani kwamba mtaingia Peponi na bado hamjapewa mitihani ya vita na mambo mazito? Haitapatikana kwenu kuingia Peponi tu, hivi hivi, mpaka mjaribiwe na Awajuwe Allah Mtukufu, ujuzi ulio wazi kwa viumbe, wale wapiganao jihadi kati yenu katika njia Yake na wenye subira ya kupambana na maadui.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net