Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 141

Aal-i-Imraan 3:141

آل عمران

وَلِيُمَحِّصَ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَيَمْحَقَ ٱلْكَـٰفِرِينَ

Maana

Na pia ili Mwenyezi Mungu awasafishe walioamini na awafutilie mbali makafiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na pia ili Mwenyezi Mungu awasafishe walio amini na awafutilie mbali makafiri. [141]

[141] Kwa huku kushindwa kwa muda, Mwenyezi Mungu anawasafisha jamaa Waumini, na anawat'ahirisha kutokana na wale wenye nyoyo mbaya na imani dhaifu, na wenye kueneza moyo wa kushindwa na wasiwasi; na kwa hivyo ndio anaung'olea mbali ukafiri na makafiri wenyewe pia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kushindwa huku kulikotokea katika vita vya Uhud kulikuwa ni kuwafanyia mtihani, kuwasafisha Waumini, kuwatakasa na wanafiki na ni maangamivu kwa makafiri.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net