Aal-i-Imraan 3:140
آل عمرانإِن يَمْسَسْكُمْ قَرْحٌ فَقَدْ مَسَّ ٱلْقَوْمَ قَرْحٌ مِّثْلُهُۥ ۚ وَتِلْكَ ٱلْأَيَّامُ نُدَاوِلُهَا بَيْنَ ٱلنَّاسِ وَلِيَعْلَمَ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَيَتَّخِذَ مِنكُمْ شُهَدَآءَ ۗ وَٱللَّهُ لَا يُحِبُّ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Ikiwa mtaguswa na majeraha, basi kwa hakika hao watu wengine walikwishapatwa na majeraha mfano wake. Na siku za namna hii tunawaletea watu kwa zamu, ili Mwenyezi Mungu awajue wale walioamini na awateue miongoni mwenu wanaokufa kwa ajili ya Dini (Mashahidi). Na Mwenyezi Mungu hawapendi madhalimu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kama yamekupateni majaraha, basi na hao watu wengine yamewapata majaraha mfano wa haya. Na siku za namna hii tunaweletea watu kwa zamu, ili Mwenyezi Mungu awapambanue walio amini na awateuwe miongoni mwenu mashahidi. Na Mwenyezi Mungu hawapendi madhaalimu; [140]
[140] Ingawa katika vita vya Uhud wameuwawa au kujuruhiwa vibaya baadhi yenu na kwa hayo mkaathirika nafsi zenu, lakini msilegee na kuhuzunika. Kwani hao makhasimu zenu yaliwapata kama hayo katika vita vya Badri. Nyakati za ushindi huendeshwa na Mwenyezi Mungu kwa watu kama apendavyo, pengine hawa hushinda, na pengine hawa, ili awatie mtihani na kuwajaribu Waumini, awateuwe wenye kusimama imara juu ya Imani yao, na apate kuwatukuza baadhi yao kwa kuwafisha mashahidi katika Sabili Llahi. Na Mwenyezi Mungu hawapendi washirikina wenye kudhulumu na wangashinda kwa kusaidiwa na wengineo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Iwapo yatawapata, enyi Waumini, majaraha au mauaji kwenye vita vya Uḥud, na mkahuzunika kwa hilo, washirikina pia walipatwa na majaraha na mauaji kama hayo katika vita vya Badr. Hizo ni siku Allah Mtukufu huzigeuza kati ya watu: wakati mwengine kushinda na wakati mwengine kushindwa. Kwani katika hayo kuna hekima, mpaka yadhihiri yale Aliyoyajua Allah Mtukufu hapo azal (kale isiyokuwa na mwanzo), ili Allah Mtukufu Ampambanue aliyekuwa mkweli wa Imani na asiyekuwa mkweli, na ili Awakirimu watu miongoni mwenu kwa kuwafanya wafe mashahidi. Na Allah Mtukufu Hawapendi waliozidhulumu nafsi zao na wakakaa kwa kuacha kupigana katika njia Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net