Aal-i-Imraan 3:139
آل عمرانوَلَا تَهِنُوا۟ وَلَا تَحْزَنُوا۟ وَأَنتُمُ ٱلْأَعْلَوْنَ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ
Wala msilegee, wala msihuzunike, kwani nyinyi ndio wa juu ikiwa nyinyi ni Waumini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala msilegee, wala msihuzunike, kwani nyinyi ndio wa juu mkiwa ni Waumini. [139]
[139] Wala nyinyi msilegelege mkadhoofika katika Jihadi Fi Sabili Llahi kwa yanayo kupateni, na wala msihuzunike kwa wanao uliwa miongoni mwenu, kwani nyinyi kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na Imani yenu na nguvu za Haki mnayo ipigania mko juu. Ushindi ni wenu ikiwa Imani yenu ni ya kweli, na maadamu mtadumu nayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wala msidhoofike, enyi Waumini, kupigana na maadui wenu, wala msihuzunike kwa yaliyowapata huko Uhud. Na nyinyi ndio washindi na mwisho mwema ni wenu iwapo mtamuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mtafuata Sheria Zake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net