Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 138

Aal-i-Imraan 3:138

آل عمران

هَـٰذَا بَيَانٌ لِّلنَّاسِ وَهُدًى وَمَوْعِظَةٌ لِّلْمُتَّقِينَ

Maana

Huu ni ubainisho kwa watu wote, na ni uongofu, na mawaidha kwa wacha Mungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hii ni bayana kwa watu wote, na ni uwongofu, na mawaidha kwa wachamngu. [138]

[138] Kwa kutajwa sifa za Waumini na kueleza shani ya Mwenyezi Mungu iliyo pita kwa walio kwisha tangulia lipo Bayana na Uwongozi kwa watu wafuate njia ya kheri, na kuwaachisha njia ya shari.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hii Qur’ani ni ufafanuzi uliyo wazi na ni uongozi kwenye njia ya haki na ni ukumbusho ambao nyoyo za wachamungu zainyenyekea. Nao (hao wachamungu) ni wale wanaomuogopa Allah Mtukufu. Wamehusishwa nayo (hiyo Qur’ani kuwa nyoyo zao zinainyenyekea na kuikubali) kwa kuwa wao ndio wanaofaidika nayo, si wengine.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net