Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 137

Aal-i-Imraan 3:137

آل عمران

قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِكُمْ سُنَنٌ فَسِيرُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ فَٱنظُرُوا۟ كَيْفَ كَانَ عَـٰقِبَةُ ٱلْمُكَذِّبِينَ

Maana

Tayari zimepita kabla yenu nyendo nyingi. Basi tembeeni katika ulimwengu na muangalie vipi ulikuwa mwisho wa wanaokanusha.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kabla yenu zimepita nyendo nyingi; basi tembeeni katika ulimwengu muangalie vipi ulikuwa mwisho wa wanao kanusha. [137]

[137] Enyi Waumini, kabla yenu shani ya Mwenyezi Mungu imewapitia kaumu zilizo kadhibisha kwa mapuuza yao. Mwenyezi Mungu akawashika kwa madhambi yao. Basi zingatieni vipi yalikuwa matokeo ya vitendo vya walio kadhibisha.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Anawazungumzia Waumini walipopatwa na mikasa siku ya vita vya Uḥud kwa kuwaliwaza kwamba wamepita kabla yao ummah wengi ambao waumini kati yao walitahiniwa kwa kupigana na makafiri na ukawa ushindi ni wao. Basi, tembeeni katika ardhi mkizingatia yale yaliyowafika wale waliomkanusha Allah Mtukufu na Mtume Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net