Aal-i-Imraan 3:136
آل عمرانأُو۟لَـٰٓئِكَ جَزَآؤُهُم مَّغْفِرَةٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَجَنَّـٰتٌ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ خَـٰلِدِينَ فِيهَا ۚ وَنِعْمَ أَجْرُ ٱلْعَـٰمِلِينَ
Hao malipo yao ni kufutiwa dhambi kutoka kwa Mola wao Mlezi, na Bustani zipitazo mito chini yake. Humo watadumu, na bora zaidi ni ujira wa watendao (wema).
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hao malipo yao ni msamaha kwa Mola wao Mlezi, na Bustani zipitazo mito kati yake. Humo watadumu, na mwema mno ujira wa watendao. [136]
[136] Basi hao wenye kusifika kwa sifa hizi ujira wao ni maghfira makubwa kutokana na Mola wao Mlezi, Mwenye kumiliki mambo yao yote, na Bustani zipitazo mito kati ya miti yake, na humo watadumu daima. Na hayo ni malipo ya neema kubwa ilioje kwa watendao amri za Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hao waliosifiwa kwa sifa hizo, malipo yao ni kwamba Allah Mtukufu Atayasitiri madhambi yao na watapata mabustani ya Peponi ambayo maji tamu yatakuwa yanapita chini ya miti yake na majumba yake ya fahari, ilhali ya kukaa humo milele; hawatotoka humo kamwe. Na malipo bora ya wenye kutenda mema ni msamaha na Pepo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net