Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 129

Aal-i-Imraan 3:129

آل عمران

وَلِلَّهِ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ ۚ يَغْفِرُ لِمَن يَشَآءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَآءُ ۚ وَٱللَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

Maana

Na ni vya Mwenyezi Mungu vyote vilivyo katika mbingu na vilivyo katika ardhi. Yeye humfutia dhambi amtakaye na humwadhibu amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ni vya Mwenyezi Mungu vyote vilivyomo katika Mbingu na vilivyomo katika Ardhi. Yeye humsamehe na humuadhibu amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Msamehevu Mwenye kurehemu. [129]

[129] Bila ya shaka vitu vyote vilioko katika Mbingu na katika Ardhi ni vya Mwenyezi Mungu peke yake, kwa kuviumba na kuvimiliki. Na Yeye ndiye Mwenye uwezo juu ya kila kitu, kila kitu kimo mikononi mwake. Yeye humsamehe ampendaye na akamuadhibu amtakaye. Lakini kusamehe kwake ndiko kulio karibu zaidi, na rehema yake ni ya kutarajiwa sana zaidi. Kwani Yeye hakika ni mwingi wa kusamehe na kurehemu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ni vya Allah Mtukufu Pekee vilioko mbinguni na vilioko ardhini; Anamsamehe Amtakaye kati ya waja Wake kwa rehema Zake na Anamuadhibu Amtakaye kwa uadilifu Wake. Allah Mtukufu ni Mwenye kuyasamehe madhambi ya waja Wake na ni Mwenye huruma kwao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net