Aal-i-Imraan 3:130
آل عمرانيَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَأْكُلُوا۟ ٱلرِّبَوٰٓا۟ أَضْعَـٰفًا مُّضَـٰعَفَةً ۖ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ
Enyi mlioamini! Msile riba mkizidisha juu kwa juu. Na mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kufaulu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio amini! Msile riba mkizidisha juu kwa juu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kufanikiwa. [130]
[130] Enyi mlio amini! Mkikopesha msichukue katika deni ila rasilmali yenu tu. Msifanye kuzidisha juu ya deni faida ya kuzidi mwaka kwa mwaka ikawa kuzidi juu kwa juu. Msiyale mali ya watu kwa upotovu. Hakika nyinyi mtaongokewa na mtafuzu pindi mkiepukana na riba, ikiwa ndogo au kubwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkazifuata Sheria Zake kivitendo, tahadharini na aina zote za riba na msichukue katika mkopo zaidi ya rasilmali zenu, hata kama ni kidogo. Basi itakuwaje iwapo ziada hiyo itaongezeka kila ufikapo muda wa kulipa deni? Na muogopeni Allah Mtukufu kwa kujilazimisha kufuata Sheria Zake ili mpate kufaulu duniani na Akhera.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net