Aal-i-Imraan 3:128
آل عمرانلَيْسَ لَكَ مِنَ ٱلْأَمْرِ شَىْءٌ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ فَإِنَّهُمْ ظَـٰلِمُونَ
Wewe huna chochote katika jambo hili. Ama atawakubalia toba au atawaadhibu, kwani wao hakika ni madhalimu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wewe huna lako jambo katika haya - ama atawahurumia au atawaadhibu, kwani wao ni madhaalimu. [128]
[128] Huna lako katika ninayo wafanyia waja wangu, kwani mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu. Ama atawasamehe kwa Imani, au atawaadhibu kwa kuuwawa na hizaya na mateso ya Siku ya Kiyama, kwani hao ni madhaalimu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Huna, ewe Mtume, katika mambo ya waja chochote kile. Bali mambo yote ni ya Allah Mtukufu, Peke Yake, Asiyekuwa na mshirika. Na huenda, baadhi ya hawa waliokupiga vita, vifua vyao vikaufungukia Uislamu, wakasilimu na Allah Mtukufu Akazikubali toba zao. Na yule atakayesalia katika ukafiri wake, Allah Mtukufu Atamuadhibu duniani na Akhera kwa sababu ya udhalimu wake na uadui wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net