Aal-i-Imraan 3:127
آل عمرانلِيَقْطَعَ طَرَفًا مِّنَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ أَوْ يَكْبِتَهُمْ فَيَنقَلِبُوا۟ خَآئِبِينَ
Ili akate sehemu katika wale waliokufuru, au awahizi; wapate kurejea nyuma hali ya kuwa wameambulia patupu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Haya ni kwa ajili awakate sehemu katika walio kufuru, au awahizi wapate kurejea nyuma nao wamepwelewa. [127]
[127] Naye Mwenyezi Mungu amekupeni ushindi ili wateketee baadhi ya wale walio kufuru kwa kuuwawa, au wadhalilike na awakasirishe kwa kushindwa na aibu na hizaya, wapate kurejea nao wameemewa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na ilikuwa nusura ya Allah Mtukufu katika vita vya Badr ni kwa ajili Apate kukiangamiza kikundi cha makafiri kwa kuuawa na yule atakayeokoka na kifo kati yao, basi atarudi akiwa na huzuni, apatwe na dhiki za nafsi yake na unaonekana kwake utwevu na aibu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net