Aal-i-Imraan 3:126
آل عمرانوَمَا جَعَلَهُ ٱللَّهُ إِلَّا بُشْرَىٰ لَكُمْ وَلِتَطْمَئِنَّ قُلُوبُكُم بِهِۦ ۗ وَمَا ٱلنَّصْرُ إِلَّا مِنْ عِندِ ٱللَّهِ ٱلْعَزِيزِ ٱلْحَكِيمِ
Na Mwenyezi Mungu hakufanya haya isipokuwa iwe ni bishara kwenu, na ili nyoyo zenu zipate kutua kwa hilo. Na nusura haitoki isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu, Mwenye hekima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Mwenyezi Mungu hakufanya haya ila kuwa ni bishara kwenu, na ili nyoyo zenu zipate kutua. Na msaada hautoki isipo kuwa kwa Mwenyezi Mungu, Aliye tukuka, Mwenye nguvu na Mwenye hikima. [126]
[126] Na wala Mwenyezi Mungu hakujaalia huko kukuleteeni msaada wa Malaika ila iwe ni bishara tu kwenu ya ushindi, na zipate kutulia nyoyo zenu. Na hapana ushindi ila unao tokana na Mwenyezi Mungu Mwenye Kushinda wote, ambaye anapanga kila kitu kwa pahala pake, na anaye wapangia mambo waja wake Waumini.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Allah Mtukufu Hakuuleta msaada huu wa Malaika isipokuwa ni kwa ajili ya kuwapa bishara kwa msaada huo na ili nyoyo zenu zitulie na ziwe nzuri kwa ahadi ya Allah Mtukufu kwenu. Na msaada wa hakika unatoka kwa Allah Mtukufu, Mwenye kushinda Ambaye Hashindwi, Mwenye hekima katika uendeshaji mambo Wake na matendo Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net