Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 125

Aal-i-Imraan 3:125

آل عمران

بَلَىٰٓ ۚ إِن تَصْبِرُوا۟ وَتَتَّقُوا۟ وَيَأْتُوكُم مِّن فَوْرِهِمْ هَـٰذَا يُمْدِدْكُمْ رَبُّكُم بِخَمْسَةِ ءَالَـٰفٍ مِّنَ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةِ مُسَوِّمِينَ

Maana

Kwani! Ikiwa mtavumilia na mkamcha Mungu, na hata maadui wakiwajia mara hii, basi hapo Mola wenu Mlezi atakusaidieni kwa Malaika elfu tano wenye alama maalumu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kwani! Ikiwa mtavumilia na mkamchamngu na hata maadui wakikutokeeni kwa ghafla, basi hapo Mola wenu Mlezi atakusaidieni kwa Malaika elfu tano wanao shambulia kwa nguvu. [125]

[125] Ndio! Msaada huo unakutosheni. Na pindi mkivumilia vita, na mkashikilia uchamngu, na hata maadui zenu wakikutokeeni kwa ghafla, Mola wenu Mlezi atawaongeza hao Malaika mpaka wafike elfu tano ili kukupeni nguvu.wakikutokeeni kwa ghafla, Mola wenu Mlezi atawaongeza hao Malaika mpaka wafike elfu tano ili kukupeni nguvu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ndio, unawatosha nyinyi msaada huu. Na kuna bishara nyingine kwenu, iwapo mtakuwa na subira ya kupambana na maadui zenu na mkamuogopa Allah Mtukufu kwa kuyatenda Aliyowamrisha na kuyaepuka Aliyowakataza. Na watakuja makafiri wa Maka kwa haraka kupigana na nyinyi, wakidhani kwamba wao watawamaliza. Allah Mtukufu Atawapa nyinyi msaada wa Malaika elfu tano wakiwa wamejitia alama zilizo wazi, wao na farasi wao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net