Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 124

Aal-i-Imraan 3:124

آل عمران

إِذْ تَقُولُ لِلْمُؤْمِنِينَ أَلَن يَكْفِيَكُمْ أَن يُمِدَّكُمْ رَبُّكُم بِثَلَـٰثَةِ ءَالَـٰفٍ مِّنَ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةِ مُنزَلِينَ

Maana

Ulipowaambia Waumini: Je, haiwatoshi kwamba Mola wenu Mlezi awasaidie kwa Malaika elfu tatu walioteremshwa?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ulipo waambia Waumini: Je, haitakutosheni ikiwa Mola wenu atakusaidieni kwa Malaika elfu tatu walio teremshwa? [124]

[124] Ushindi ulipatikana Mtume alipo waambia Waumini: Haitatosha kukutulizeni nafsi zenu Mola wenu Mlezi ikusaidieni kwa Malaika elfu tatu watakao letwa ili kukutieni nguvu?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kumbuka, ewe Nabii, yale yaliyowahusu Masahaba wako kwenye vita vya Badr pindi walipoona uzito katika nafsi zao kwa kuwa Makureshi wamepata msaada wa kivita, na Sisi tukakuletea Wahyi uwaambie, «Kwani hauwatoshi msaada wa Mola wenu wa kuwaletea Malaika elfu tatu walioteremshwa kutoka mbinguni mpaka kwenye sehemu ya vita wakawa wanawapa moyo na wanapigana pamoja na nyinyi?»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net