Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 123

Aal-i-Imraan 3:123

آل عمران

وَلَقَدْ نَصَرَكُمُ ٱللَّهُ بِبَدْرٍ وَأَنتُمْ أَذِلَّةٌ ۖ فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ

Maana

Na Mwenyezi Mungu alishawanusuru huko Badri hali ya kuwa nyinyi ni wanyonge. Basi mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kushukuru.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Mwenyezi Mungu alikwisha kunusuruni katika Badri nanyi mlikuwa wanyonge. Basi mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kushukuru. [123]

[123] Mwenyezi Mungu amewakumbusha Waumini ile neema ya nusura aliyo wapa katika vita vya Badri waliposubiri. Akawahakikishia kuwa Yeye ndiye aliye wapa ushindi katika vita vile na ingawa walikuwa wachache na wapungufu wa silaha; akawataka wamt'ii kuwa ni shukrani kwa neema hiyo. Badri ipo mwendo wa kiasi ya maili 120 kusini magharibi ya Madina. Mpambano hapo baina ya Waislamu na Makureshi ulikuwa siku ya Jumaane 17 Ramadhani mwaka wa pili wa Hijra (13 Machi 624 B.K.). Mtume s.a.w. na Masahaba wake walitoka Madina taarikh 8-9 ya Ramadhani mwaka wa pili wa Hijra (5 Machi 624 B.K.) Idadi ya wapiganaji wa Kiislamu katika vita hivi ilikuwa kiasi watu mia tatu au zaidi kidogo, na Washirikina walizidi mara tatu kuliko hao. Mwenyezi Mungu alitimiza ahadi yake katika vita hivi, Waumini wakashinda juu ya kuwa ni wachache, kwa kuwa Imani yao juu ya haki na uadilifu ilikuwa kubwa. Na kuungwa mkono na Mwenyezi Mungu pamoja na kuwa na moyo wenyewe kulikuwa ni sababu za ushindi kuliko wingi wa watu na ubora wa silaha. Ushindi huu ulio dhaahiri ukawa ndio sababu ya kuenea Neno la Imani na kutukuka likawa juu. Na hichi ni chanzo cha yaliyo kuja baadae, na kivuli cha Uislamu kikatanda Arabuni kote, na kisha kwengineko ulimwenguni.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika Allah Mtukufu Aliwanusuru nyinyi, enyi Waumini, katika Badr juu ya maadui zenu washirikina pamoja na uchache wa idadi yenu na vifaa vyenu. Kwa hivyo, muogopeni Allah Mtukufu kwa kutekeleza amri Zake na kujiepusha na makatazo Yake, ili mpate kushukuru neema Zake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net