Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 122

Aal-i-Imraan 3:122

آل عمران

إِذْ هَمَّت طَّآئِفَتَانِ مِنكُمْ أَن تَفْشَلَا وَٱللَّهُ وَلِيُّهُمَا ۗ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ ٱلْمُؤْمِنُونَ

Maana

Makundi mawili miongoni mwenu yalipoingiwa na woga kuwa watashindwa - na hali Mwenyezi Mungu ndiye Kipenzi Mlinzi wao. Na kwa Mwenyezi Mungu tu, na wategemee Waumini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Makundi mawili miongoni mwenu yakaingiwa na woga kuwa watashindwa - na hali Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wao; na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu. [122]

[122] Ilipo tokea kuwa vikundi viwili vya Waumini kuingiwa na khofu ya kushindwa na wakataka kurejea nyuma, Mwenyezi Mungu aliwalinda akawapa moyo wa kuthibiti, wakasonga mbele katika vita. Kwani hakika Mwenyezi Mungu ndiye mwenye utawala katika mambo yao mawili, na ndiye wa kuwalinda na kuwawezesha kwa kuwapa tawfiqi. Basi Waumini nawachukue funzo kutokana na haya, na wamtegemee Yeye ili awanusuru.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kumbuka, ewe Mtume, yale mambo yaliyowahusu kina Banû Salimah na Banû Ḥãrithah wakati walipowaza kurudi nyuma, wao na kiongozi wao, mnafiki Abdullãh bin Ubayy bin Salûl, kwa kuogopa kukutana na adui. Lakini Allah Mtukufu Aliwalinda na Akawahifadhi wakaenda pamoja na wewe wakimtegemea Allah Mtukufu. Na kwa Allah Mtukufu, Peke Yake, wajitegemeze Waumini.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net