Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 121

Aal-i-Imraan 3:121

آل عمران

وَإِذْ غَدَوْتَ مِنْ أَهْلِكَ تُبَوِّئُ ٱلْمُؤْمِنِينَ مَقَـٰعِدَ لِلْقِتَالِ ۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ

Maana

Na pale ulipotoka asubuhi kwa ahali zako ili uwapange Waumini kwenye vituo kwa ajili ya vita. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na pale ulipo toka asubuhi, ukaacha ahali zako uwapange Waumini kwenye vituo kwa ajili ya vita - na Mwenyezi Mungu anasikia na anajua. [121]

[121] Na hebu taja Ewe Nabii! Pale ulipo toka asubuhi mapema ukaacha ahali zako, watu wako wa nyumbani, ukenda mpaka Uhud kwa makusudi ya kuwaweka Waumini katika makao yao kwa ajili ya vita. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia kauli zenu, ni Mwenye kuzijua niya zenu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kumbuka,ewe Mtume, pindi ulipotoka nyumbani kwako, ukiwa umevaa mavazi ya vita, huku wazipanga safu za Masahaba wako, na unamuweka kila mmoja mahali pake ili kukutana na washirikina katika vita vya Uḥud. Na Allah Mtukufu ni Mwenye kuzisikia kauli zenu, ni Mwenye kuvijua vitendo vyenu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net