Aal-i-Imraan 3:120
آل عمرانإِن تَمْسَسْكُمْ حَسَنَةٌ تَسُؤْهُمْ وَإِن تُصِبْكُمْ سَيِّئَةٌ يَفْرَحُوا۟ بِهَا ۖ وَإِن تَصْبِرُوا۟ وَتَتَّقُوا۟ لَا يَضُرُّكُمْ كَيْدُهُمْ شَيْـًٔا ۗ إِنَّ ٱللَّهَ بِمَا يَعْمَلُونَ مُحِيطٌ
Ikikuguzeni heri, inawawia vibaya. Na ikikupateni shari, wanaifurahia. Na nyinyi mkisubiri na mkamcha Mwenyezi Mungu, havitawadhuru kitu vitimbi vyao. Hakika, Mwenyezi Mungu ameyazingira yote wayatendayo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ikikupateni kheri huwaudhi. Na ikikupateni shari wanafurahia. Na nyinyi mkisubiri na mkajizuilia, hila zao hazitakudhuruni kitu. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kuyazunguka yote wayatendayo. [120]
[120] Nyinyi mkipata neema, kama vile kushinda vitani na ngawira, wao husikitika. Mkipata msiba kama ukame na kushindwa, wao hufurahia msiba wenu. Lakini nyinyi mkisubiri juu ya maudhi yao, na mkajizuilia na kule kuwafanya urafiki mliko katazwa, basi maudhi yao na uadui wao hautakudhuruni kitu. Kwani Yeye Aliye tukuka anavijua vyema vitimbi wanavyo vifanya, wala Yeye hashindwi kukulindeni nao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na miongoni mwa uadui wa watu hawa ni kwamba nyinyi, enyi Waumini, mpatwapo na jambo jema la ushindi au ngawira, wao hupatwa na butwaa na huzuni; iwapo mtapatwa na maudhi ya kushindwa au upungufu wa mali, watu na matunda, wao hulifurahia hilo. Na mkiwa na subira juu ya yaliyowafika na mkamuogopa Allah Mtukufu katika yale Aliyowaamrisha na Akawakataza nayo, hautawadhuru udhia wa vitimbi vyao. Na Allah Mtukufu ni Mwenye kuyazunguka yote wanayoyafanya hao makafiri ya uharibifu na Atawalipa kwayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net