Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 119

Aal-i-Imraan 3:119

آل عمران

هَـٰٓأَنتُمْ أُو۟لَآءِ تُحِبُّونَهُمْ وَلَا يُحِبُّونَكُمْ وَتُؤْمِنُونَ بِٱلْكِتَـٰبِ كُلِّهِۦ وَإِذَا لَقُوكُمْ قَالُوٓا۟ ءَامَنَّا وَإِذَا خَلَوْا۟ عَضُّوا۟ عَلَيْكُمُ ٱلْأَنَامِلَ مِنَ ٱلْغَيْظِ ۚ قُلْ مُوتُوا۟ بِغَيْظِكُمْ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ

Maana

Nyinyi ndio hawa mnawapenda watu hao, wala wao hawawapendi. Nanyi mnaviamini Vitabu vyote. Na wanapokutana nanyi husema: 'Tumeamini.' Na wanapokuwa peke yao, wanawaumia vidole kwa chuki. Sema: Kufeni na chuki yenu! Hakika, Mwenyezi Mungu anayajua vyema yale yaliyo katika vifua.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hivyo basi nyinyi ndio mnawapenda watu hao, wala wao hawakupendeni. Nanyi mnaviamini Vitabu vyote. Na wanapo kutana nanyi husema: Tumeamini. Na wanapo kuwa peke yao wanakuumieni vidole kwa chuki. Sema: Kufeni kwa chuki yenu! Hakika Mwenyezi Mungu anayajua yaliomo vifuani. [119]

[119] Enyi nyinyi Waumini! Mnawapenda hawa makafiri na wanaafiki kwa ajili ya ujamaa, au urafiki au mapenzi tu. Na wao, lakini, hawakupendeni kwa sababu ya kuing'ang'anilia dini yao. Na nyinyi mnaamini Vitabu vyote vilivyo teremka kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Wanapo kutana nanyi hujitia imani ili kukudanganyeni. Na wakisha kuacheni huziuma ncha za vidole vyao kwa chuki na kukasirika. Ewe Nabii! Waambie: Endeleeni na hiyo chuki yenu mpaka mfe! Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kuyajua yanayo fichikana vifuani, na atakulipeni kwavyo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Huu ndio ushahidi wa makosa yenu kwa kuwapenda wao. Nyinyi mnawapenda na mnawafanyia wema, na wao hawawapendi. Na wanawabebea nyinyi uadui na chuki, ilhali nyinyi mnaviamini vitabu vyote vilivyoteremshwa, kikiwemo kitabu chao, na wao hawakiamini kitabu chenu. Basi vipi mtawapenda? Na wanapokutana na nyinyi wanasema kinafiki, «Tumeamini na tumesadiki.» Na wanapokuwa faragha, wenyewe kwa wenyewe, yaonekena wana kero na masikitiko. Hapo huwa wakiziuma ncha za vidole vyao, kutokana na hasira kali walionayo juu ya mshikamano wa Waislamu, kuwa neno lao ni moja, kuwa Uislamu umepata nguvu na kuwa wao wamekuwa wanyonge kwa sababu ya kupata nguvu Uislamu.Waambie, ewe Mtume, «Kufeni kwa hasira zenu kali mlizonazo. Hakika Allah Mtukufu ni Mwenye kuyaona yanayofichwa ndani ya vifua na Atamlipa kila mmoja kwa aliyoyatanguliza ya kheri au ya shari».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net