Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 118

Aal-i-Imraan 3:118

آل عمران

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَتَّخِذُوا۟ بِطَانَةً مِّن دُونِكُمْ لَا يَأْلُونَكُمْ خَبَالًا وَدُّوا۟ مَا عَنِتُّمْ قَدْ بَدَتِ ٱلْبَغْضَآءُ مِنْ أَفْوَٰهِهِمْ وَمَا تُخْفِى صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ ۚ قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ ٱلْـَٔايَـٰتِ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْقِلُونَ

Maana

Enyi mlioamini! Msiwafanye wandani wenu kuwa watu wasiokuwa katika nyinyi. Hawataacha kuwafikishia lolote la kuwadhuru. Wanapenda mngepata taabu. Imekwishadhihirika chuki yao kutoka katika midomo yao. Na yanayofichwa na vifua vyao ni makubwa zaidi.Tumekwishawabainishia Ishara ikiwa nyinyi mnatumia akili.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio amini! Msiwafanye wasiri wenu watu wasio kuwa katika nyinyi. Hawataacha kukufanyieni ubaya. Wanayapenda yanayo kudhuruni. Imekwisha fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayo ficha vifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekwisha kubainishieni Ishara ikiwa nyinyi mtayatia akilini. [118]

[118] Enyi mlio amini! Msitafute kuwafanya marafiki wa ndani watu wasio wa Dini yenu mkatumai msaada kwao, na mkawa mkiwapa siri zenu. Hao hawatoacha kuyafisidi mambo yenu, kwani wao wanapenda mno kukutieni taabuni na kukudhuruni kwa madhara makubwa. Zimekwisha dhihiri ishara za bughdha yao kukuchukieni nyinyi katika kuropokwa ndimi zao. Na yaliyo ficha nyoyo zao ni makubwa zaidi. Tumekwisha kuonyesheni alama za kumtambua rafiki na adui kama nyinyi ni watu wa akili na utambuzi wa kweli.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkazifuata Sheria Zake kivitendo, msiwafanye makafiri kuwa ni wategemewa, kinyume cha Waumini, mkawa mnawapa siri zenu. Kwani wao hawakomi kuziharibu hali zenu, na wanayafurahia madhara na maovu yanayowafika. Zimedhihiri chuki nyingi katika maneno yao. Na yanayofichwa na nyoyo zao ya uadui kwenu ni makubwa zaidi na ni mazito. Kwa hakika, tushawaelezea nyinyi alama na hoja za uovu wao ili mpate kuwaidhika na muwe na tahadhari, iwapo mnayatia akilini mawaidha ya Allah Mtukufu, amri Zake na makatazo Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net