Aal-i-Imraan 3:117
آل عمرانمَثَلُ مَا يُنفِقُونَ فِى هَـٰذِهِ ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا كَمَثَلِ رِيحٍ فِيهَا صِرٌّ أَصَابَتْ حَرْثَ قَوْمٍ ظَلَمُوٓا۟ أَنفُسَهُمْ فَأَهْلَكَتْهُ ۚ وَمَا ظَلَمَهُمُ ٱللَّهُ وَلَـٰكِنْ أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ
Mfano wa vile wanavyovitoa katika uhai wao wa duniani ni kama upepo ambao ndani yake kuna baridi ya barafu, ukalipiga shamba la kaumu waliozidhulumu nafsi zao, basi ukaliharibu. Na Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu, bali wao wenyewe wanazidhulumu nafsi zao.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mfano wa vile wanavyo vitoa katika uhai wao wa duniani ni kama upepo ambao ndani yake ipo baridi ya barafu, ukalisibu shamba la watu walio dhulumu nafsi zao, ukaliteketeza. Na Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu, bali wao wenyewe wanadhulumu nafsi zao. [117]
[117] Hakika hali ya wanacho kitoa makafiri duniani kuwa ni sadaka au cha kuwakaribisha mbele ya Mwenyezi Mungu Akhera mfano wake, kwa kuwa ni kazi bure katika ujira wa vitendo, ni kama hali ya shamba la watu walio jidhulumu nafsi zao kwa ukafiri na maasi. Shamba hilo likakumbwa na upepo wenye baridi kali ya barafu, likateketea shamba lote kuwa ni malipo yao. Wala Mwenyezi Mungu siye aliye wadhulumu ujira wa kazi yao, lakini ni wao wenyewe ndio walio jidhulumu nafsi zao kwa kufanya yaliyo sabibisha hayo. Nayo ni kuzipinga dalili na ushahidi wa Imani na kumkufuru Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mfano wa wanachokitoa makafiri, katika mambo ya kheri, katika maisha haya ya ulimenguni na thawabu wanazozitumaini, ni mfano wa upepo ulio na baridi kali uliovuma juu ya mashamba ya watu waliokuwa wanangojea kwa hamu matokeo mema ya upepo huo. Na kwa sababu ya madhambi yao, upepo huo haukubakisha chochote. Na makafiri hawa, hawatapata thawabu huko Akhera. Na Allah Mtukufu hatakuwa Amewadhulumu kwa hilo, lakini ni wao walijidhulumu nafsi zao kwa ukafiri wao na kuasi kwao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net