Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 116

Aal-i-Imraan 3:116

آل عمران

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لَن تُغْنِىَ عَنْهُمْ أَمْوَٰلُهُمْ وَلَآ أَوْلَـٰدُهُم مِّنَ ٱللَّهِ شَيْـًٔا ۖ وَأُو۟لَـٰٓئِكَ أَصْحَـٰبُ ٱلنَّارِ ۚ هُمْ فِيهَا خَـٰلِدُونَ

Maana

Hakika, wale waliokufuru, hazitawafaa kitu mali zao wala watoto wao mbele ya Mwenyezi Mungu. Na hao ndio watu wa Motoni. Wao watadumu humo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale walio kufuru hazitawafaa kitu mali zao wala watoto wao mbele ya Mwenyezi Mungu. Na hao ndio watu wa Motoni - humo watadumu. [116]

[116] Wale walio kufuru, mali yao na wangayatoa kuwa ni fidia hayatowafaa kitu, wala watoto wao na wangawataka msaada hawatoweza kuwasaidia hata chembe kuwakinga na adhabu ya Mwenyezi Mungu katika Akhera. Na hawa ndio walio lazimika kuingia Motoni na waselelee humo.(wadumu)

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale waliozikufuru aya za Allah Mtukufu na wakawakanusha Mitume Wake, mali yao wala watoto wao havitawatetea wao kivyovyote wasipatwe na adhabu ya Allah Mtukufu, duniani wala Akhera. Hao ni watu wa Motoni watakaodumu humo pasi na kutoka.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net