Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 115

Aal-i-Imraan 3:115

آل عمران

وَمَا يَفْعَلُوا۟ مِنْ خَيْرٍ فَلَن يُكْفَرُوهُ ۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌۢ بِٱلْمُتَّقِينَ

Maana

Na heri yoyote wanayoifanya, basi hawatanyimwa malipo yake. Na Mwenyezi Mungu anawajua wacha Mungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kheri yoyote wanayo ifanya hawatanyimwa malipwa yake. Na Mwenyezi Mungu anawajua wachamngu. [115]

[115] Kheri yoyote wanayo ifanya watu hao hawatonyimwa thawabu zake. Na Mwenyezi Mungu amezizunguka kwa kuzijua na kuziweza hali zao na malipo yao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kitendo chochote, kichache au kingi, kati ya vitendo vyema yatakayofanywa na kikundi hiki kilichoamini, hakitapotea mbele ya Allah Mtukufu. Bali watashukuriwa na watapewa malipo yake. Allah Mtukufu Anawajua zaidi wacha Mungu ambao wametenda mema na wakajitenga na yaliyoharamishwa kwa kutaka radhi za Allah Mtukufu na kutaka thawabu Zake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net