Aal-i-Imraan 3:114
آل عمرانيُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ وَيَأْمُرُونَ بِٱلْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ ٱلْمُنكَرِ وَيُسَـٰرِعُونَ فِى ٱلْخَيْرَٰتِ وَأُو۟لَـٰٓئِكَ مِنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ
Wanamwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na wanaamrisha mema na wanakataza maovu, na wanakimbilia katika mambo ya heri. Na hao wako miongoni mwa walio wema.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wanamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na wanaamrisha mema na wanakataza maovu na wanakimbilia katika mambo ya kheri. Na hao ndio miongoni mwa watenda mema. [114]
[114] Wanaamini kweli kuwepo Mwenyezi Mungu, na kuwa Yeye ni Mmoja tu. Wanaamini Mitume wote, hawamuabudu ila Mwenyezi Mungu. Na wanaamini kuwa itafika Siku ya Kiyama; wanaamrisha ut'iifu kwa Mwenyezi Mungu, na wanakataza maasi, na wanawania kutenda mambo ya kheri. Hawa kwa Mwenyezi Mungu huhisabiwa miongoni mwa watenda wema.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wanamuamini Allah Mtukufu na Siku ya Mwisho, wanaamrisha mambo ya kheri yote na wanakataza aina zote za shari na wanakimbilia kufanya mema. Hao ni miongoni mwa waja wa Allah Mtukufu wema.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net