Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 113

Aal-i-Imraan 3:113

آل عمران

لَيْسُوا۟ سَوَآءً ۗ مِّنْ أَهْلِ ٱلْكِتَـٰبِ أُمَّةٌ قَآئِمَةٌ يَتْلُونَ ءَايَـٰتِ ٱللَّهِ ءَانَآءَ ٱلَّيْلِ وَهُمْ يَسْجُدُونَ

Maana

Wote hao si wamoja. Miongoni mwa Watu wa Kitabu kuna watu waliosimama barabara, wanasoma Aya za Mwenyezi Mungu nyakati za usiku, nao wanasujudu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wote hao si sawa sawa. Miongoni mwa Watu wa Kitabu wamo watu walio simama baraabara, wanasoma Aya za Mwenyezi Mungu nyakati za usiku, na pia wanasujudu. [113]

[113] Watu wa Kitabu si wote sawa sawa. Miongoni mwao wapo walio simama msimamo mwema, wa uadilifu, wanakisoma Kitabu cha Mwenyezi Mungu nyakati za usiku wakiswali.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Waliopewa Vitabu hawako sawa: kati yao liko kundi lifuatalo njia iliyolingana sawa juu ya amri ya Allah Mtukufu, lenye kumuamini Mtume Wake Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, na ambalo watu wake wanasimama usiku wakizisoma aya za Qur’ani tukufu na wakielekea kwa Allah Mtukufu kwa kumuomba katika Swala zao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net